Tuesday, 24 July 2012

MAOMBI HALALI in KISWAHILI

MAOMBI HALALI
Raia wa Kongo wanaomba kusitishwa kwa uhalifu unaofanywa na Rwanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 Kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa New York ;
 Kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa New York ;
Kwa mataifa wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Toka miongo miwili, raia wa Kongo wameteswa na uvamizi wa mara kwa mara kutoka Rwanda. Kinyume chake, ni mauaji, na uharibifu wa familia. Alikadhalika, uvamizi huo una yagombanisha kabila moja dhidi ya lingine na unahatarisha ujio wa taifa zima.
Kumeripotiwa ukeukaji mkubwa wa haki za binadamu, maelfu ya wanawake wamebakwa na zaidi ya wakongomani milioni sita(6) wameuwawa na kuwaacha maelfu ya wajane na watoto yatima. Uhalifu huo unaendelea leo kufuatia ripoti ya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa (N°S /2012/348) na viungo vyake ambayo vinaelezea ya kwamba :
Rwanda ndio imeunda kikundi cha M23;
 Rwanda inatoa silaha, inarahisisha na kutoa uungaji mkono wa kiufundi kwa kikundi cha M23 kutoka kwenye ardhi yake.;
Rwanda inawasajili watoto na wakimbizi na kuwapa mafunzo wapiganaji wa zamani wa FDLR kwa ajili ya kikundi cha M23;
 Rwanda inajiingiza katika maswala ya ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kuwasajili wanasiasa kadhaa wa Kongo kwa ajili ya kundi la M23;
 Jeshi la Rwanda (RDF) limekueko kwenye ardhi ya Kongo likiwaunga mkono waasi wa kikundi cha M23;
 Rwanda inatoa msaada wa vifaa na wa kifedha kwenye makundi mengineo yasiyo halali yeye silaha nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo;
Rwanda inashirikiana na wapiganaji wa kikundi FDLR;
 Rwanda inakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa kuhusu marufuku (embargo) ya silaha na watu kwenye Kanda la Maziwa Makuu;
 Rwanda imekuwa kimbilio la wahalifu wa vita wanaotafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (CPI).
Uvamizi usio wa haki na usioeleweka unahatarisha juhudi za maridhiano (masikilizano) na ujenzi wa taifa la Kongo. Unafuatiwa na uhalifu wa mipaka ambao bado kuwahi kutokea, na uporaji mwingi wa rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Kutokana na uvamizi wa wazi wa ardhi ya Kongo, SISI raia wa Kongo, tunaomba :
1. Kuhamasishwa kwa kikosi cha MONUSCO ili kuunga mkono Jeshi wa FARDC kwa ajili ya kusimamisha mara moja uvamizi, uporaji wa rasilimali na ubakaji wa wanawake wa Kongo;
2. Kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya kisheria kwa mahalifu wote wa kivita waliotajwa kwenye ripoti ya Umoja wa Mataifa;
3. Kukamatwa na kufikishwa mbele ya Mahakama wahalifu wote wa kivita kwa ajili ya uhalifu wote uliofanywa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na mahalifu wote wanaotawanyika Kongo na katika nchi jirani;
4. Kutupiliwa mbali ombi la ugombeaji wa Rwanda kama mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutokana na ukeukaji wake wa kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa;
5. Kutekelezwa bila kuchelewa kwa hatua zote za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya amani nchini Kongo.
Kulingana na hayo yaliopo hapo juu, tunapinga kuweko kwa mazungumzo yeyote na mahalifu wa milele na vile vile jaribio la kuigawa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Inatolewa Kinshasa, siku, mwezi na mwaka ufuatao.

No comments:

Post a Comment